SWALA AGM Notice 2019 (swahili version)

29th January, 2019

All News, Annual General Meeting News, SWALA News

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SWALA OIL AND GAS (TANZANIA) PLC

TAARIFA INAYOTOLEWA HAPA kwamba mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa Swala Oil and Gas (Tanzania) Plc utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere International Conference Centre, Jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa tarehe 1 Februari 2019, kuanzia saa 04:00 asubuhi mpaka saa 06:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

MAELEZO MUHIMU

  1. Mjumbe anayetaka kuhudhuria mkutano huu anapaswa kuja na moja kati ya vitambulisho vifuatavyo: Nakala ya risiti ya bohari (Depository Receipt), nakala ya hati ya kusafiria, Kadi
    ya mpiga kura au Kitambulisho cha Taifa.


  2. Mjumbe mwenye haki ya kuhudhuria na kupiga kura katika mkutano ana haki ya kuchagua mwakilishi wa kuhudhuria na kupiga kura kwa niaba yake kwa mujibu wa masharti na taratibu
    za ibara ya muongozo wa kampuni. Fomu ya mwakilishi iwasilishwe katika ofisi za kampuni zilizosajiliwa kabla ya siku ya jumatatu tarehe 30 mwezi Januari 2019, saa 04:00 Asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)


  3. Wajumbe wanaotaka kuhudhuria mkutano huu wanapaswa kuhudhuria kwa gharama zao wenyewe. Nakala za taarifa za fedha zilizo fanyiwa ukaguzi za mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2017 na fomu za mwakilishi wa Mjumbe/mwanahisa zitapatikana katika ofisi za Swala Oil & Gas (Tanzania) Plc, Oyster Plaza, Ghorofa ya pili, Barabara ya Haile Selassie, Jijini Dar es salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28 Januari 2019.