NMB Bank Yazindua Hatifungani ya JASIRI
8th February, 2022
NMB JASIRI ni hatifungani kwa ajili ya wawekezaji wote , wakubwa na wadogo, na kwa mtu yoyote ili mradi yuko tayari kuwekeza kwenye benki ya NMB.
Mapato ya hatifungani hii yatatumika kusaidia utoaji wa mikono nafuu kwa biashara na makampuni yanayomilikiwa au kusimamiwa na wanawake, pamoja na biashara ambazo bidhaa ama huduma zake zinamnufaisha mwanamke.
Hatifungani hii:
- Itakupatia riba nzuri ya asilimia 8.5% kwa mwaka
- Kiwango cha chini cha ununuaji ni TZS 500,000/=
- Ununuzi ni kupitia tawi lolote la benki ya NMB, au kupitia madalali waliosajiliwa na Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
Pakua fomu ya kuwekeza katika hatifungani hii kupitia link ifuatayo kisha wasilisha fomu ikiwa imeijaza kikamilifu kupitia barua pepe yetu solomonstockbrokers@solomon.co.tz